Friday, April 29, 2011

Mimi Kibaruani

In the office.

In the field,in one of our branches.

In one of the Kongamano.

Mpunga wa leo 29.04.2011

Kwa wale walioalikwa tu,hii ndo njia ya kufikia huko,

Monday, April 18, 2011

Kambi ya Makapera yapata pigo

Ijumaa ya tarehe 15/04/2011 Kambi ya makapera ilipata pigo kubwa baada ya Mdau wake maarufu na wa siku nyingi Khatibu Mackenga kufunga pingu za maisha na Bi Fatma Ally nyumbani kwa Wazazi wa Bi Harusi huko Mbezi kwa Msuguri na kufuatiwa na bonge moja la M'sherehe uliofanyika katika ukumbi wa Briged Mess Lugalo jeshini siku ya tarehe 16/04/2011.

"Eenh enh wewe kweli hautamletea mauzauza Binti yangu,mbona macho yako yanaonekana kama mwingi wa habari vile" ni kama Mzee Ally Juma anamwambia Bwana harusi vile,wakati akimfungisha ndoa Bwana Khatibu kwa binti yake Bi Fatma mbele ya usimamizi wa mashekhe.

"Mbona sioni pa ku'sign jamani"...."hapa - una'sign hapa,sign faster isije kutokea mtu akachomoza na pingamizi"
Bwana harusi aki'speed up tukio la kuanguka signature katika cheti cha ndoa.

Katika tukio hilo la kufunga ndoa kwa Bwana Khatibu na Bi Fatma,mambo mengi yasiyo ya kawaida yalijitokeza ikiwemo hili la Wapambe wa bwana harusi kuvunja kanzu na viremba bila kusahau vikoi vya kuazima kama Mpambe wa kushoto kabisa katika picha hii hapa juu anavyoonekana.

Maharusi wakiwa na wapambe wao mara baada ya kufunga ndoa,Wapambe wa kwanza kushoto kwa waliosimama na kukaa ni baadhi ya wale waliotafuta kuendana na dhana nzima ya shughuli yenyewe ndo maana hata ukaaji wao na muonekano wao kwa ujumla umekuwa ni tofauti na wenzao

Wakiwa katika nyuso za furaha ni Bwanana Bibi Khatibu Makenga ndani ya ukumbi wa Brigade Mess lugalo jeshini katika sherehe ya kuwapongeza kwa uamuzi wao wakufunga ndoa.

Blog hii inapenda kuwatakia maharusi maisha mema yenye baraka na mafanikio kichele.

Monday, April 11, 2011

Wafalme warejea.

Sehemu ya umati wa Mashabiki wa Dar Young Africans waliofurika katika Viunga vya Uwanja wa ndege wa kimataifa jana kuipokea team yao ikitokea Mwanza walipokuwa wakicheza mchezo wao wa mwisho.


Sehemu ya Mabasi yaliyobeba mashabiki wa Yanga yaliyokuwa kwenye Msafara wa mapokezi ya Wachezaji wa team hiyo waliokuwa wakitokea Jijini Mwanza ambapo waliichapa team ya Toto Africans na Kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.

Pikipiki maarufu kama bodaboda nazo zilikuwepo kuongoza msafara huo.

Hammer kibanda wazi iliyokuwa imewabeba Viongozi na nahodha wa Yanga aliyesimama na Kombe juu.

Mzee wa matokeao ya kushangaza Sam(wa ukweli) Timbe,Kocha mkuu wa Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya Tanzania Bara akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ku'drop Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere wakitokea Jijini Mwanza.

Huyu ndiye Mwali/kombe la ligi kuu ya Tanzania bara ambalo team ya Yanga walilitwaa juzi baada ya kuichapa Toto Africans 3 - 0.

Mabingwa kusaka kabumbu Young Africans almaarufu kama Yanga katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wao na Kombe lao katika makao makuu ya Club hiyo jana.

Picha kwa hisani ya Global Publishers na Michuzi blog.

YANGA bingwa 2011

Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuizamisha Toto Africa ya Jijini Mwanza kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mabingwa wa zamani Simba ambayo nao walikuwa wakicheza na Majimaji(iliyomaliza na wachezaji 8) katika uwanja wa uhuru Jijini Dar walifanikiwa kuibuka na ushindi wa Magoli 4-1 lakini hata hivyo magoli hayo hayakutosheleza kuwawezesha kutetea Taji hilo walilitwaa mwaka jana.
Yanga na Simba zote zimemaliza ligi hiyo zikiwa na pointi 49 huku Yanga ikiwa na tofauti ya magoli (Goal Difference) ya 25 wakati Simba ina 24.
Mabao ya Yanga katika mchezo wa jana yalifungwa katika kipindi cha pili na Nurdin Bakari aliyetia nyavuni magoli mawili na Davis Mwape moja.

Nahodha wa team ya Yanga ambaye pia ni nahodha wa team ya Taifa ya Tanzania Shadrack Nsajigwa akiwa na Kombe la Ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom pamoja na wachezaji wenzake mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh Abas Kandoro.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza wakati Yanga wakikabidhiwa Kombe hilo kule CCM Kirumba, kombe lililokuwa limeandaliwa uwanja wa Uhuru kwaajili ya kuwakabidhi Simba endapo wangeibuka na magoli ya kutosha ilibidi lirudishwe TFF baada ya Mnyama kushindwa kuibuka kidedea.

Vi'model wakirudisha Kombe kwa Wahusika TFF baada ya aliyeandaliwa kukabidhiwa endapo angeshinda vizuri kushindwa kufanya hivyo.

Wednesday, April 6, 2011

Mikonoz!

Mikonoz!
Hivi ndo ninavyoweza kusema,kipindi hicho sijui tulikuwa na akili gani,ilikuwa tukipiga picha lazima tunyooshe mikono,mikonoz!!! hii ilikuwa year 2000 Najja High School na Masela wangu to mention but few Walter,Fidelis,Octavian,Marehemu Justine(RIP Brother),Sule,Danny,Maz,Mcharo na wengineo.

Sunday, April 3, 2011

The World's biggest family!

  • Ziona Chana lives with all of them in a 100-room mansion
  • His wives take it in turns to share his bed
  • It takes 30 whole chickens just to make dinner

He is head of the world's biggest family - and says he is 'blessed' to have his 39 wives.

Ziona Chana also has 94 children, 14-daughters-in-law and 33 grandchildren.

They live in a 100-room, four storey house set amidst the hills of Baktwang village in the Indian state of Mizoram, where the wives sleep in giant communal dormitories.

The full monty: The Ziona family in its entirety with all 181 members.

You treat this place like a hotel: With 100 rooms the Ziona mansion is the biggest concrete structure in the hilly village of Baktawng.

Feeling peckish? The senior ladies of the Chana family show what it takes just to make a meal.

The wives and him: Mr Ziona Chana poses with his 39 wives at their home in Baktawang, Mizoram, India.

Shared bedroom: A look inside the four-storey mansion, Chhuanthar Run - The House of the New Generation.

Ama kweli Duniani kuna mambo,ukitaka kuipata habari hii kwa undani zaidi tembelea:-

Friday, April 1, 2011

Usela unapopitiliza huwa haipendezi

Jumamosi ya tarehe 26 March 2011 kulitolewa tuzo kwa Wanamuziki waliofanya vizuri katika msimu wa 2010/2011 maarufu kama Kilimanjaro Music Awards.
Katika sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee,Msanii Abas Hamis Kinzasa Maarufu kama 20% alifanikiwa kutwaa tuzo 5 peke yake na kuweka record ya Msanii aliyetwaa tuzo nyingi kwa mpigo tokea tuzo hizo zianzishwe miaka 12 iliyopita.
Msanii huyo hata hivyo hakuwepo hiyo siku ya kutunukiwa hizo tuzo na aliwakilishwa na Produce wake ManWater/Man Maji - Combination/Combinenga.
Inaelezwa kuwa 20% alikuwa Tabora kikazi na alikuwa akifuatilia ugawaji wa tuzo hizo kwenye Television.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za chini ya Carpet Global Publishers,Mfalme wa Rhymes mwaka 2004 Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele ambaye ni Swaiba mkubwa wa 20% aliamua kumuandalia bonge la part Mshikaji wake ili kumpongeza kwa ushindi wake wa kishindo,hivyo basi akitokea Tabora 20% ali'drop Morogoro kwa Mshikaji wake kwaajili ya kushiriki katika Part hiyo.
Ni katika picha zilizochukuliwa katika Part hiyo,20% alifanikiwa kunijuza upande wake mwingine,mwonekano wake na vitendo alivyo'reportiwa kuvifanya yeye,Swaiba wake na waalikwa wengine katika Part hiyo vimenisikitisha sana.


Pombe,Sigara na Bhangi vinatajwa kutawala shughuli hiyo.
Blog hii inamtambua 20% kama mmoja wa Wasanii wakali kwa sasa hivi hapa nchini na yeye hana budi kujitambua,nchi nzima inakubali kazi zake na ndo maana akafanikiwa kuibuka kidedea kwenye categories zote alizokuwa anashindania,hivyo basi ninapenda kumshauri ajaribu kujiweka katika muonekano unaokubalika na hadhira na siyo kupiga mguu mmoja Sandle na mwingine Ndala zote choka.
Napenda kuwakumbusha 20% na Swaiba zake kuwa Usela siyo kutooga au kuvaa jeans isiyowahi kugusa maji 2 years,ukiulizwa "Mimi Msela,nipo Simple" hakuna cha U'simple hapo.

Na hizo bhangi zao wanazovuta inabidi ziwe na limit hata kama ndo zinawapa steam za kutunga mashairi yenye maujumbe.

Picha kwa hisani ya Global Publishers.

Thursday, March 31, 2011

Watanzania wanapochoka na maisha bora ya kila mmojawao

Mtanzania huyu baada ya kushindwa kununua sukari iliyokuwa inauzwa Tsh 2000/= aliamua kuja na ujumbe wake huu.

Hawa kwa hayo machache waliyoya'list hapo waliamua kuja na proposal hii.

Na hawa baada ya kuchunguzachunguza na kupata habari ya kazi nzuri zilizofanyika huko Libya waliamua kuja na ujumbe huu.

Thursday, March 24, 2011

Down the memory!

At Najja High School,Kampala Uganda,together with my fellow Tanzanians schoolmates to mention but few Harold,Dickson,Anorld,Mabamba,God,Jack,Msase and others.