Tetemeko hilo ambalo linasemekana kuwa na ujazo wa Magnitude 9 linasemwa kuwa ni tetemeko kubwa kuliko yote kuwahi kutokea katika nchi ya Japan,huku likishika nafasi ya 5 kwa ukubwa kuwahi kutokea katika Sayari hii ya Dunia tokea kuanza kuchukuliwa record kwa matukio ya aina hii hapa Duniani.
Zifuatazo ni baadhi ya Picha za athari ya Tetemeko hilo lililoambatana na Tsunami:-

Nyumba zikiwa zimefagiwa na Tsunami katika Mji wa Natori Kaskazini Mashariki mwa Japan.
Nyumba magari na rasilimali nyingine zikiwa zimeharibiwa vibaya na Tsunami iliyosababishwa na Tetemeko la ardhi kubwa katika Mji wa Miyagi Kaskazini mwa Japan
Nyumba zikiwaka moto huku mawimbi ya Tsunami yakipiga kama kawaida katika Mji wa Miyagi Kaskazini mwa Japan.
Miti ikiwa imepigwa shuruba na kuangukia barabarani kuziba njia karibu na Mji wa Iwaki Kaskazini Mashariki mwa Japan.
Magari yakiwa yamepondwa na ukuta uliokuwa umeangushwa na tetemeko la ardhi huko katika Mji wa Mito Ibaraki.
Kimbunga chenyewe hakikuona sababu ya kutofautisha Parking za Magari na za Ndege - Airport,hapa ndege kutoka Sendai Airport zikiwa zimekusanywa sehemu 1 na magari pembezoni mwa Mji huo
Hizi nazo zikatoswa baharini.
Na hizi zikakusanywa mpaka pembezoni mwa ufukwe wa Sendai
Katika sura ya huzuni watu wakishuhudia maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika bandari ya Kesenuma Mjini Miyagi.

0 comments:
Post a Comment