"Eenh enh wewe kweli hautamletea mauzauza Binti yangu,mbona macho yako yanaonekana kama mwingi wa habari vile" ni kama Mzee Ally Juma anamwambia Bwana harusi vile,wakati akimfungisha ndoa Bwana Khatibu kwa binti yake Bi Fatma mbele ya usimamizi wa mashekhe.
"Mbona sioni pa ku'sign jamani"...."hapa - una'sign hapa,sign faster isije kutokea mtu akachomoza na pingamizi"Bwana harusi aki'speed up tukio la kuanguka signature katika cheti cha ndoa.
Katika tukio hilo la kufunga ndoa kwa Bwana Khatibu na Bi Fatma,mambo mengi yasiyo ya kawaida yalijitokeza ikiwemo hili la Wapambe wa bwana harusi kuvunja kanzu na viremba bila kusahau vikoi vya kuazima kama Mpambe wa kushoto kabisa katika picha hii hapa juu anavyoonekana.
Maharusi wakiwa na wapambe wao mara baada ya kufunga ndoa,Wapambe wa kwanza kushoto kwa waliosimama na kukaa ni baadhi ya wale waliotafuta kuendana na dhana nzima ya shughuli yenyewe ndo maana hata ukaaji wao na muonekano wao kwa ujumla umekuwa ni tofauti na wenzao
Wakiwa katika nyuso za furaha ni Bwanana Bibi Khatibu Makenga ndani ya ukumbi wa Brigade Mess lugalo jeshini katika sherehe ya kuwapongeza kwa uamuzi wao wakufunga ndoa.Blog hii inapenda kuwatakia maharusi maisha mema yenye baraka na mafanikio kichele.

0 comments:
Post a Comment