Katika sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee,Msanii Abas Hamis Kinzasa Maarufu kama 20% alifanikiwa kutwaa tuzo 5 peke yake na kuweka record ya Msanii aliyetwaa tuzo nyingi kwa mpigo tokea tuzo hizo zianzishwe miaka 12 iliyopita.
Msanii huyo hata hivyo hakuwepo hiyo siku ya kutunukiwa hizo tuzo na aliwakilishwa na Produce wake ManWater/Man Maji - Combination/Combinenga.
Inaelezwa kuwa 20% alikuwa Tabora kikazi na alikuwa akifuatilia ugawaji wa tuzo hizo kwenye Television.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za chini ya Carpet Global Publishers,Mfalme wa Rhymes mwaka 2004 Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele ambaye ni Swaiba mkubwa wa 20% aliamua kumuandalia bonge la part Mshikaji wake ili kumpongeza kwa ushindi wake wa kishindo,hivyo basi akitokea Tabora 20% ali'drop Morogoro kwa Mshikaji wake kwaajili ya kushiriki katika Part hiyo.
Ni katika picha zilizochukuliwa katika Part hiyo,20% alifanikiwa kunijuza upande wake mwingine,mwonekano wake na vitendo alivyo'reportiwa kuvifanya yeye,Swaiba wake na waalikwa wengine katika Part hiyo vimenisikitisha sana.
Blog hii inamtambua 20% kama mmoja wa Wasanii wakali kwa sasa hivi hapa nchini na yeye hana budi kujitambua,nchi nzima inakubali kazi zake na ndo maana akafanikiwa kuibuka kidedea kwenye categories zote alizokuwa anashindania,hivyo basi ninapenda kumshauri ajaribu kujiweka katika muonekano unaokubalika na hadhira na siyo kupiga mguu mmoja Sandle na mwingine Ndala zote choka.
Napenda kuwakumbusha 20% na Swaiba zake kuwa Usela siyo kutooga au kuvaa jeans isiyowahi kugusa maji 2 years,ukiulizwa "Mimi Msela,nipo Simple" hakuna cha U'simple hapo.
Na hizo bhangi zao wanazovuta inabidi ziwe na limit hata kama ndo zinawapa steam za kutunga mashairi yenye maujumbe.
Picha kwa hisani ya Global Publishers.

1 comments:
Tabia bi kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili...!!
Tukilemaa na huu usemi still 2takuwa kama hao masela hapo...!!
Post a Comment